Mahakama ya kadhi / islamic court
- A. Ferrari
- 6 juil. 2016
- 1 min de lecture
Tizama video kisha jibu maswali yafuatayo.
1. Bunge la katiba limekubali kuingiza mahakama ya kadhi katika katiba?
a) Sio, haikukubali.
b) Ndio, limekubali.
2. Waziri Mkuu Mhe.Mizengo ametolea uafafanuzi lengo la Mahakama ya Kadhi akisema itahusika na utatuzi wa masuala ya kifamilia kama vile mirathi na ndoa.
a) Kweli.
b) Si kweli.
3. Mahakama ya kadhi pia itahusika na mambo ya jinai?
a) Kweli itahusika na mambo hayo.
b) Sio, haitahusika na mambo hayo.
4. Waziri mkuu amesema kuwa serikali imedhamiria kuweka utaratibu wa kutambua shughuli zinazofanywa na mahakama ya kadhi.
a) Kweli, amesema hivo.
b) Si kweli, hajasema hivo.
5. Kulingana na waziri mkuu, kwa nini serikali inataka kutambua chumbo hiki ?
a) Kwa sababu si kinyume cha katiba na ni haki kwa Waislamu kuwa na mahakama yao.
b) Kwa sababu kunao watu wasiotambua mahakama ya kawaida katika maswala ya kifamilia.
c) Kwa sababu waislamu ni wengi sana nchini Tanzania na ni muhimu kuwafurahisha kwa sababu ya uchaguzi ujazo.
d) Kwa sababu ya shinikizo kubwa ya umma ya Waislamu wanaoishi Tanzania.
Commenti