Mbona kuna uhaba wa sukari
- A. Ferrari ( BBC video)
- 25 mai 2016
- 1 min de lecture
Msamiati
mfumuko wa bei : inflation
uagizaji kutoka nje: import
kuuza nje: export
biasharanje: export
uzalishaji wa ndani : local production
upungufu: deficit
miwa: sugar cane
Maana tofauti za “kuwa”
The verb/ auxilary kuwa usually expresses the concept of to be or to have ( kuwa na), it is also used to form compound verbs but it can also have other meanings.
kwa kuwa : kwa sababu
kuwa (baada ya kitenzi): kwamba
inakuwaje ( pia ilikuwaje na itakuwaje): je hii inawezekana? ( pia ni salamu: habari!)
ikiwa: kama
ijapokuwa (or ijapo) : though, while, despite the fact of.
Zoezi la kwanza : Jaza sentensi zifuatazo na maneno hayo: ikiwa – kuwa – kwa kuwa – ijapokuwa -inakuwaje
1. Mwuzaji wa chai anasema ……….. uhaba wa sukari umemwathiri sana.
2. …………………… sukari iagizwe kutoka Brazil na bado iwe rahisi kuliko sukari ya hapa.
3. Wananchi wanalalamika ……….... sukari haipatikani kirahisi na ikipatikana inauzwa kwa bei ghali.
4. Watu wamezoea kununua chai mia mbili, ………. unawaambia chai ni mia tatu wanaacha, hawataki kununua.
5. ................... bei ya sukari imepanda sana, mwuzaji anaendelea kuuza chai mia mbili tu.
Zoezi la pili: andika mukhtasari kuhusu mambo yanayozungumzwa kwenye video, jaribu kutumia kwa kuwa, kuwa, ikiwa n. k.
Comments