top of page

Tohara na Uketetaji

  • A. Ferrari
  • 22 mars 2016
  • 3 min de lecture

Msamiati:

-balehe : reach puberty

bikira : virgin

hedhi : menstruation

imani potofu : myth, distorted belief

-keketa : mutilate

kinembe : clitoris

kosa la jinai : crime

maambukizi : infection, contamination

ngariba : circumciser

ngono : sex

sehemu za siri : genital organs

shida ya mkojo : urinary problem

shirika la afya duniani : World Health Organisation

-tahiri : circumcise

tendo la ndoa : the act of marriage

tohara : circumcision

tohara kwa wasichana : excision

ubikira : virginity

ukeketaji: Female Genital Mutilation (FGM)

ukiukwaji wa haki Za mtoto: violation of children rights

upasuaji: operation

uvuja damu : bleeding

viungo vya uzazi: reproductive organs

Mfuko wa Kimataifa wa Watoto/ Mfuko wa Watoto wa Imoja wa Mataifa / Shirika la Kuwahudmia Watoto la Umoja wa Mataifa : UNICEF

Tizama video kisha chagua jibu sahihi.

1 - Maandalizi ya sherehe au siku kuu gani yanaendelea uwanjani mtaani Kawangware?

A. Maandalizi ya sherehe ya busa na tohara ya mtoto wa kabila la Waluya.

B. Maandalizi ya tohara yaani hali ya kutokuwa na najisi ya mtoto katika kabila la Waluya.

C. Maandalizi ya tohara yaani harusi ya mtoto wa miaka 16 katika kabila la Waluya.

D. Maandalizi ya tohara yaani siku ya kuzaliwa ya mtoto aliye na miaka 16 katika kabila la Waluya.

2 - Shughuli gani hufanyika kwa maandalizi ya siku kuu au sherehe hiyo katika utamaduni wa Waluya?

A. Shughuli kama kutayarisha busa, yaani pombe wa kiutamaduni, kuwatembelea watu wa ukoo, kuimba, kupasha tohara, kumpa mtoto maneno ya kumtia moyo hufanyika kwa maandalizi ya sherehe hiyo.

B. Shughuli kama kujua kama mtoto ana roho au la, majaribio ya nyimbo, na kutayarisha busa, kuita ngariba kutembelea wazee wa kijiji hufanyika kwa maandalizi ya sherehe hiyo.

C. Shughuli kama kutayarisha busa, yaani kinywaji kikali, kutembelea watu wa ukoo, kumpa mtoto jina la msinde, kutia visu makali kumpa mtoto maneno ya kumtia moyo hufanyika kwa maandalizi ya sherehe hiyo.

D. Shughuli kama kutayarisha busa, yaani pombe ya kienyeji, kuwatembelea watu wa ukoo, kutia visu makali , kumpa mtoto maneno ya kumtia moyo, hufanyika kwa maandalizi ya sherehe hiyo.

3 - Sentensi hiyo anataka kukutana na kisu cha ngariba humaanisha nini? Ngariba ni nini?

A. Anataka kutahiriwa. Ni mtu ambaye anafanya kazi ya kutahirisha.

B. Anataka kufanya tohara. Ni mtu anayetayarisha sherehe hiyo.

C. Anataka kufanya tohara. Ni mtu anayefanya kazi ya kutengeneza pombe.

D. Anataka kukata na kuchinja mbuzi au mnyama mwingine. Ni mtu anayechinja wanyama.

4 - Mtoto anapewa zawadi gani kwa ajili ya sherehe hiyo? Kwa kawaida, sherehe hiyo hufanyika wapi lakini mara hii hufanyika wapi ? Kwa nini wameamua hivo?

A. Mtoto anapewa busa, na kisu kikali kuchinja mnyama kwa ajili ya sherehe hiyo. Kwa kawaida sherehe hizo hufanyika mashambani , mara hii inafanyika jijini kwa sababu mtoto alitaka sherehe hiyo isiwe sherehe ya ukabila.

B.Mtoto anapewa mnyama hai au nyama ya mnyama aliyechinjwa kwa ajili ya sherehe hiyo. Kwa kawaida sherehe hizo hufanyika mashambani , mara hii inafanyika Nairobi kwa sababu mtoto alitaka sherehe hiyo isiwe sherehe ya ukabila.

C. Mtoto anapewa busa na mnyama hai kwa ajili ya sherehe hiyo. Kwa kawaida sherehe hizo hufanyika mashambani , mara hii inafanyika Nairobi kwa sababu mtoto alitaka sherehe hiyo isiwe sherehe ya ukabila.

D. Mtoto anapewa pombe aina ya busa na kisu kukata nyama kwa ajili ya sherehe hiyo. Kwa kawaida sherehe hizo hufanyika mashambani , mara hii inafanyika jijini kwa sababu mtoto alitaka sherehe hiyo iwe sherehe ya ukabila.

5 - Kulingana na maelezeo hayo, shughuli gani hufanyika siku kuu ikifika?

A. Baada ya kukesha, mtoto anapelekwa mtoni alfajiri anavua nguo na anatumbukizwa kwenye maji baridi, na kupakwa udongo mwilini mzima halafu shughuli ya tohara hufanyika, ikiisha ngariba anapiga filimbi.

B. Baada ya kunywa busa, mtoto anapelekwa mtoni anavua nguo na anatumbukizwa kwenye maji baridi halafu shughuli ya tohara hufanyika mtoto anamchinja mnyama ikiisha ngariba anapiga filimbi.

C. Baada ya kukesha, mtoto anapelekwa mtoni, anavua nguo na anatumbukizwa kwenye maji baridi na kupakwa udongo baridi halafu shughuli ya tohara hufanyika ikiisha mtoto anapiga filimbi.

D. Baada ya kunywa busa, mtoto anapelekwa mtoni anavua nguo na anatumbukizwa kwenye maji baridi na kupakwa udongo na ngariba halafu shughuli ya tohara hufanyika ikiisha ngariba anapiga filimbi.


Comments


  • Facebook Clean Grey
  • Twitter Clean Grey
  • LinkedIn Clean Grey
bottom of page