0:02 / 1:13 Asili yao ni Goa lakini ni Watanzania
- A. Ferrari (BBC video)
- 23 avr. 2016
- 1 min de lecture
Msamiati/ vocabulary:
kizazi: generation
asili: origin
Mreno: Portuguese
juzijuzi: recently
wenyewe: themselves
mwenyeji: native
jitambua: present/introduce oneself
Sarufi/grammar
The auxiliary -wahi means "to have a chance to" in affirmative sentences.
Aliwahi kufanya kazi kule.
He had the chance to work there.
With the ME tense marker, -wahi means "ever"
Umewahi kwenda Kenya? have you ever gone to Kenya?
The verb -wahi used with the negative present tense means never.
Sijawahi kupanda ndege. I never flew on a plane.
The verb -auxliary with other negative tenses means "not to have a chance to"
Hakuwahi kumwona. He didn't have a chance to see him.
Hatawahi kumwona: He will not have a chance to see him.
Tizama video kisha jibu maswali.
1. Goa ni wapi?
a) Ni kisiwa cha India.
b) Ni mkoa wa India.
c) Ni mji wa Tanzania.
d) Ni kijiji cha Tanzania.
2. Wagoa hawa wamekuwa Tanzania tangu muda mrefu?
a) Ndio.
b) Hapana, wamekuja juzi juzi.
3. Waliletwa Tanzania na nani?
a) Walikuja wenyewe.
b) Waliletwa na Watanzania.
c) Waliletwa na Waarabu
d) Waliletwa na Wareno.
4. Wanaishi vipi?
a) Kama Waindia.
b) Kama Watanzania.
c) Kama Waarabu.
d) Kama Waingereza.
5. Elliot amezaliwa Tanzania?
a) Ndio, amezaliwa Tanzania.
c) Hapana, amezaliwa India.
6. Wazazi wake wamezaliwa wapi?
a) Uingereza.
b) Tanzania.
c) India.
d) Goa.
7. Elliot anasema kwamba akienda India anakuwa:
a) Kama wenyeji.
b) Kama wageni.
8. Akienda India anazungumza lugha gani?
a) Kiswahili.
b) Lugha ya Goa.
c) Kihindi.
d) Kiingereza.
9. Amekwenda mara ngapi Goa?
a) Ameenda mara mbili.
b) Huenda kila mwaka.
c) Amekwenda mara moja.
d) Amekwenda mara kumi.
Comments