HOTUBA / SPEECH
- rekebisho
- 29 févr. 2016
- 2 min de lecture
Tizama video kisha jibu maswali yafuatayo. Watch the video then answer the question below.
1. Mwalimu J. Nyerere anasema Watanzania wanataka nini?
a) Wanataka rushwa.
b) Wanataka kubadilisha.
c) Wanataka mabadiliko.
d) Wanataka ukabila.
2. Mwalimu J. Nyerere anasema kwamba Watanzania wamechoka na nini?
a) Wamechoka na rushwa.
b) Wamechoka na dini.
c) Wamechoka na chama hiki.
d) amechoka na mabadiliko.
3. Hotuba hiyo ilifanyika kwa fursa gani?
a) Ilifanyika katika mkutano wa CCM kabla kuteua mgombea wao.
b) Ilifanyika katika mkutano wa CCM kabla uchaguzi wa urais.
c) Ilifanyika bungeni.
d) Ilifanyika kwa kusherekea miaka 20 ya CCM.
4. Mwalimu J. Nyerere anasema kwamba mgombea lazima atambue nini?
a) Lazima atambue kwamba Watanzania ni wabaguzi wa rangi.
b) Lazima atambue kwamba Watanzania wanahitaji kazi.
c) Lazima atambue kwamba Watanzania ni wafanyakazi na wakulima maskini.
d) Lazima atambue kwamba Watanzania wanafanya ubaguzi wa dini.
5. Zamani, watanzania walikuwa wakijali dini ya watu?
a) Ndio walikuwa wakijali sana dini ya watu.
b) Ndio,walikuwa wakijali lakini kidogo tu.
c) Ndio, wakati wa ukoloni wakoloni walijali sana dini ya watu.
d) La, hawakuwa wakijali dini ya watu hata kidogo.
6. Kwa mujibu wa J. Nyerere, Tanzania ilikuwa mfano Afrika Mashariki kwa sababu gani ?
a) Kwa sababu hawakuwa na ukabila.
b) Kwa sababu ya utawala bora.
c) Kwa sababu walikuwa na uchumi bora.
d) Kwa sababu walikuwa na viongozi wazuri.
7. Hotuba hiyo ilipokelewa vipi na wanachama?
a) Vizuri sana, watu wanacheka, kupiga makofi.
b) Vizuri sana, watu wanacheza na kupiga makofi.
c) Vibaya, watu wanapiga kelele.
d) Vizuri sana, watu wanacheka na kupiga kofi.
8. Nyerere anafanya hotuba hiyo na nia gani ?
a) Kuenzi chama hiki.
b) Anafanya hotuba na nia ya kusaidia nchi.
c) Kulaumu viongozi wa CCM.
d) Kuteuliwa kama mgombea wa CCM.
Comments